Tuesday, February 1, 2011

Wabunge wote wangekuwa Hivi ingekuwa Poa eh?

I always applaud New leaders, who practise new ways and think a little bit differently. January Makamba sure has a great new Idea to getting in touch with his people. To hell with ' Mikutano ya vijiji' who speaks openly there anyway nowadays....this is a new era and we do need other newer more quicker ways of doing  things. Wasiliana na Mbunge wako kwa njia ya simu!
Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya SMS Kati ya Wananchi wa Bumbuli na Mbunge wao, Ndugu January Makamba, yamezinduliwa tarehe 29 Januari 2011 kwenye Semina Elekezi aliyoitisha Mbunge huyo wa viongozi na watendaji wa vijiji na Kata wapatao 250 wa Jimbo la Bumbuli. Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika. Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu. Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi. Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana. Inawezekana ikaonekana ni gharama kubwa kwa Mbunge lakini hata haiko hivyo, ni suala ya mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu ili gharama iwe at cost na Mbunge bado anaweza kugharamia hili kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).
Wabunge wote wangekuwa hivi ingekuwa Poa eh?

No comments:

Post a Comment