Sunday, May 29, 2011

Prose: Life Like The Wind

Katika dimbwi la mawazo.
Ndani ya train masafa ya mbali
Tunasafiri na kupita ka upepo
Nyumba zinarudi nyuma, miti pia,
Kila kitu kinarudi nyuma wakati train linaenda mbele. 
Maisha, maisha! Maisha ni Kama upepo
Upepo unaovuma kwa kasi
Unakuja mbele yako kisha kila kitu kinarudishwa nyuma,
Kama ninavyo experience ndani ya hii train. 
Upepo, ni mtu wa ajabu sana.
Anaweza kukugusa na kukuacha mwili wa sisimka.
Upepo ni mwanamume asiyetabirika,
Anapenda nipuliza uso wangu kisha Kunipepea nywele.
Anaponigusa ngozi yangu sio Siri napatwaga na goosebumbs (vipele vya baridi) msisimuko usio kwepeka.
Nampenda sana huyu mwanamume upepo anapokuwa nami especially kipindi cha joto. Wakati mwili umoto na unamuhitaji kwa sana. Maani hata nikimnywa mwanamume barafu hawezi kukidhi mahitaji yote ya kuniondolea joto mwilini.

Wakati wa kurudi haikuwa the same. Mwanamume jua akielekea nyumbani kwake magharibi kaniacha peke yangu
Peke yangu njiani na Mr. Upepo na Mr. Giza. Hawa wanaume wawili wamenikumbatia kisasawa njia mzima mpaka nifikapo nyumbani kumfuata mchumba wangu taa.  Kipindi chote hiko njiani rafiki yangu kipenzi kwajina anaitwa muziki alikuwa akinifariji na kunitumbuiza kwa kazi nzuri niliyokuwa Nikifanya siku nzima ya kusomaa na kujibu maswali mbalimbali kujiandaa kwa mitihani ya kufunga mwaka kwa ajili ya kiangazi.
By Lulu Mero

No comments:

Post a Comment